Katika kutafuta
amani ya Sudan Kusini, Rais Salva Kiir amemteua mpinzani wake Riek
Machar kuwa makamu wa rais.Majeshi yanayowatii watu hawa wawili ,
walipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha watu zaidi ya
milioni moja na nusu kukimbia makazi yao.
Machar ambaye alikuwa
amehaidiwa wadhifa huo wa makamu wa raisi kama atakubali kuweka sahihi
katika makubalino ya kuleta amani ulifanyika mwezi Agosti mwaka jana
.lakini bado baadhi ya majeshi yamejigawa na kuendeleza mapigano katika
baadhi ya maeneo ya Sudan Kusini.Mtangazaji akisoma kwa sauti ya juu amri ya raisi kumteua Machar kuwa msaidizi wake,amri hiyo ilisomwa kama ifuatavyo;katika zoezi la mgawanyiko wa utawala chini ya kifungu namba 524 cha sheria cha kwanza cha makubaliano ya kufikia hatima ya mgogoro unaoendelea jamuhuri ya sudan ya kusini.
Salva Kiir,raisi wa Jamuhuri ya Sudan ya kusini amemteu Dr,Riek Machar kuwa makamu wa kwanza wa raisi ya jamuhuri ya Sudan ya Kusini kuanzia tarehe 11 Februari 2016
Post a Comment