Uganda haipaswi kuzuia upinzani, Obasanjo
Aliyekuwa rais wa
zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, ametaka pande zote pinzani katika
uchaguzi wa Uganda kujiepusha na matamshi ya uhasama.
Obasanjo
ambaye aliongoza ujumbe wa Jumuiya ya madola uliokuwa ukiangalia vigezo
vya kidemokrasia katika uchaguzi uliokamilika nchini Uganda amewashauri
viongozi wa uganda kujiepusha na makabiliano na migongano baina yao.Obasanjo alisema''Uhuru wa kujieleza kutengamana na kuwasilana na umma wa kila kiongozi sharti ulindwe na kama kuna vizuizi dhidi ya kiongozi yeyote lazima iondolewe mara moja''
Aliongezea kuwa ''dosari zilizoshuhudiwa katika uchanguzi mkuu umekuwa na madhara mabaya kwa matokeo ya ukweli haki na uwazi wa uchaguzi huo'' , lakini amesisitiza tofauti kati ya utawala na upinzani zinahitajika kusuluhiswa kupitia mazugumzo.''
- Kauli hiyo ya Obasanjo inawadia saa chache baada ya Kizza Besigye kukamatwa na polisi wa Uganda.
- Mtazamo wa Besigye kuhusu uchaguzi
Wakili wake amethibitisha habari za kukamatwa kwake.
Awali kulikuwa na habari kwamba angefika makao makuu ya Tume ya Uchaguzi kuitisha matokeo rasmi ya kina ya uchaguzi wa urais.
Post a Comment