0


Idara ya uhamiaji imezitaja nchi za China, Ethiopia na jamuhuri ya kudemokrasia ya Congo kuongoza kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji haramu hapa nchini ambpo tayri wameshakamatwa wahamiaji haramu takribani 162 na watanzania kumi na tano wanaowasaidia wahamiaji hao kuishi nchini.

Afisa uhamiaji mkoa wa Dar es Saalamu akizungumza na ITV amesema kufuatia operesheni ya kukamata wahamiaji haramu katika mkoa wa Dar es Salaam iliyofanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu mia moja na sitini na mbili kutoka nchi za China Ethiopia na DRC wakiishi nchini kinyume cha sheria na tayri wameshapelekwa mahakamani na mara baada ya kesi zao kuisha watarudishwa katika mataifa waliyotokea.

Aidha afisa huyo amebaini pia watanzani kumi na tano wamekamatwa katika operesheni hiyo kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuwatafutia wahamiaji haramu hati bandia za kuishi nchini kinyume cha sheria ambapo pia ametoa wito kwa wananchi kuacha kabisa tabia hiyo kwani ni kosa kisheria na hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kuwasaidia wahamiaji haramu kuishi nchini.

Operesheni ya kukamata wahamiaji haramu nchini kwa mkoa wa Dar es Salaam ilianza mapema tarehe 24 Decemba mwaka jana na kuwa zoezi hilo litaendelea katika manispaa ya Kinondoni wiki baada ya kumalizika katika manispaa ya Ilala hasa eneo la Kariakoo.

Post a Comment

 
Top