Kamanda
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es
Salaam, Abbas Mtemvu akimkabidhi vifaa vya michezo Katibu Kata ya Mtoni
kwa Azizi Ally vyenye thamani ya sh.800,000 kwa wenyeviti wa CCM wa
Kata mbalimbali wilayani Temeke katika Hafla fupi ya kusheherekea miaka
39 ya kuzaliwa kwa chama hicho ambapo kilele cha maadhimisho hayo
yatafanyika kesho Mkoani Singida ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Rais Mstaafu Dtk Jakaya Kikwete
Na Khamisi Mussa
Kamanda wa
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dar es Salaam,
Abbas Mtemvu ametoa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh.800,000 kwa
wenyeviti wa CCM wa Kata mbalimbali wilayani Temeke.
Mtemvu
alitoa vifaa hivyo ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya miaka 39 ya
kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo kilele chake kitaifa
kinafanyika leo mkoani Singida na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Rais
mstaafu Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mtemvu alisema lengo lake ni kuimarisha
michezo kwenye kata hizo na kuwaepusha vijana kujiingiza katika vitendo
vya kiovu na kujenga afya zao.
Post a Comment