0
Ndege ya kampuni ya Daalo nchini Somalia ilioshambuliwa
Mwalimu mmoja wa shule ya Madrasa, ametambuliwa kuwa mshukiwa aliyetekeleza shambulio la bomu ambalo lilisababisha shimo kubwa katika tanki ya mafuta ya ndege moja ya abiria nchini Somalia, iliyokuwa ikielekea nchini Djibouti, tarehe mbili Februari mwaka huu.
Abdullahi Abdisalam Borleh, alirushwa na mlipuko uliotokea katika ndege hiyo aina ya Airbus 321, wakati bomu hilo lilipolipuka muda mfupi baada ya ndege hiyo kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Mogadishu.
Maafisa wa idara ya ujasusi wanaamini kuwa Borley, ambaye anatoka eneo lililojitenga na Somalia la Somaliland, alibeba bomu hiyo kimakusudi.
 
Tundu iliosababishwa na mlipuko huo
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Al Shabaab, lilidai kuhusika na mlipuko huo, lakini halijatoa majina ya waliohusika moja kwa moja.
Hamna aliyeuawa wakati wa mlipuko huo, ambao ulitokea dakika kumi na tano baada ya ndege hiyo kupaa.
Ndege hiyo ililazimika kurejea na kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Mogadishu nchini Somalia.

Post a Comment

 
Top