0
Mamlaka ya anga ya Serikali ya Zimbabwe February 15 imetangaza kuikamata ndege ya kimarekani inayomilikiwa na Western Global Airlines iliyokuwa imeomba kutua kwa dharura katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare. Zimbabwe imekamata ndege hiyo iliyokuwa  inatoka Ujerumani ikiwa imebeba hela za Afrika Kusini (rand) na maiti.
Ndege hiyo ya mizigo aina ya MD11 iliomba kutua kwa dharura Harare ili ipate msaada wa usalama, lakini ilikuwa inaenda Afrika Kusini  na ilitua Zimbabwe ili kuomba msaada wa mafuta kabla ya kuendelea na safari yao ya Afrika Kusini. Uchunguzi wa ndege hiyo ulikuwa unaendelea.
Meneja wa mamlaka ya anga ya Zimbabwe David Chaota amethibitisha kukamatwa kwa ndege hiyo ya kampuni ya Western Global Airlines, kampuni ambayo ipo Florida Marekani, inaripotiwa kuwa ilianza kuomba kutua Msumbiji lakini ilikataliwa.

Post a Comment

 
Top