Virusi vya Zika vinasababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo
Kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya Zika kimethibitishwa barani Ulaya.
Mwanamke mmoja nchini Uhispania, ambaye alirejea nchini humo majuzi kutoka nchini Colombia amepatikana na virusi hivyo.Wizara ya afya inasema inaaminika kwamba aliambukizwa virusi hivyo akiwa nchini Colombia.
Virusi vya Zika vinaaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo na ubongo uliodumaa.
Virusi hivyo vinaenea kwa kasi mataifa ya Amerika na Shirikisho la Afya Duniani (WHO) limetangaza dharura ya kimataifa duniani.
Post a Comment