Kinondoni yaahidi mapato mara tatu ya agizo
MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob amesema wamejipanga
kuongeza ukusanyaji wa mapato mara tatu zaidi ya agizo la Wizara ya
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambalo ni Sh bilioni 48.
Pia ametawangazia kiama wakandarasi watakaolipua kazi zao, akisema hawatavumiliwa na kwamba pamoja na kuwavunjia mikataba, itawaandikia barua katika Bodi zao za Usajili wa Makandarasi (CRB), Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) na Bodi ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa hatua zaidi.
Aliyasema hayo jana Dar es Salaam mara baada ya kukabidhiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mwongozo wa Ilani na Katiba ya chama hicho, kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake ya umeya katika manispaa hiyo.
Alisema kwa mujibu wa Tamisemi, Kinondoni inatakiwa iongeze ukusanyaji wa mapato na kufikia Sh bilioni 48 kwa mwezi. “Nina uhakika kwa jinsi tulivyojipanga tutakusanya mara ya tatu ya agizo hilo, tutaanza na kubana kampuni zote zinazokwepa kodi,” alisema na kuongeza kuwa, kutokana na kukithiri kwa kampuni zinazokwepa kodi katika manispaa hiyo jumla ya Sh bilioni tano hadi 10 hupotea kila mwezi.
Kuhusu vipaumbele katika Manispaa ya Kinondoni, alisema wameanza na mkakati wa kuondokana na uchafu na tayari imeagiza malori ya kubeba taka 35 hadi 40, ujenzi wa dampo la kisasa Mabwepande na mashine za kushindilia taka.
Awali, akimkabidhi ilani na Katiba ya chama hicho kama mwongozo wa utendaji kazi akiwa Meya wa Kinondoni, Mratibu wa Kanda ya Pwani wa Chadema, Casmir Mabina, alisema mwongozo huo utamsaidia Meya huyo kutekeleza majukumu yake kulingana na matakwa ya Ilani na Katiba ya chama hicho.
Alisema katika ilani hiyo, imebainisha vipaumbele vya kufanyiwa kazi, ikiwa ni pamoja na suala la bomoabomoa katika maeneo ya mabondeni. “Tumeweka wazi kuwa sisi hatupingani na ubomoaji kwa sababu kila maendeleo yanakuja na madhara, ila tunasisitiza ubomoaji huo ufuate sheria na utu,” alisema.

Post a Comment