Kambi rasmi ya upinzani Bungeni imesema deni la taifa limeongezeka na
kufikia kiasi cha shilingi trilioni 41.5 kwa viwango vya ubadilishaji wa
fedha hivi sasa.
Mfano katika mpango wa miaka 5 iliyopita serikali iliahidi kupata umeme wa megawati 2780 ambapo kila mwaka ilitakiwa izalishe megawati 556 lakini ilizalisha megawati 344 hii inaashiria kwamba utekelezaji wa miradi haukuenda kulingana na ahadi zilizotolewa.
Kwa upande wa barabara mpango uliopita ulionyesha kutengeneza barabara kilomita 5400 ambapo hadi kipindi cha miaka 5 inamalizika serikali imeweza kujenga kilomita 2775 sawa na 53%.
Aidha kambi ya upinzani bungeni imeitaka serikali kutotegemea zaidi wahisani ila wapange miradi kulingana na vipaumbele maalum ili kuweza kuleta ufanisi.

Post a Comment