Rais
wa Simba Sport Club Evans Aveva Akikata Utepe wakati wa Uzinduzi wa
Duka la Vifaa vya Michezo akiwa Ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuuwa
Eaggroup Ndugu Iman Kajula Pamoja na Wadau wengine wa Club Hiyo.
Katika kukuza wigo wake wa mapato pamoja na upatikanaji wa vifaa, klabu ya Simba leo imezindua duka lake rasmi kwa ajili ya kuuza vifaa vya michezo vyenye chapa ya Simba.
Katika kukuza wigo wake wa mapato pamoja na upatikanaji wa vifaa, klabu ya Simba leo imezindua duka lake rasmi kwa ajili ya kuuza vifaa vya michezo vyenye chapa ya Simba.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Rais wa Simba Evans Aveva alisema “kama
mtakumbuka moja ya malengo ambayo uongozi wangu huu uliopo madarakani
ulijiwekea ni pamoja na kuongeza wigo wa mapato kupitia vyanzo vyake
vilivyopo lakini pia kuja na mkakati kabambe kwa ajili ya kuongeza na
leo wote tunakuwa mashuhuda katika kuzindua duka letu la vifaa vya
michezo. Duka ambalo litakuwa likiuza kila bidhaa ambayo inachapa Simba
hivyo wanachama na wapenzi wa Simba kuweza kujua ni wapi mahala pa
kupata vitu halisi vya Simba na kwa bei nafuu zaidi”
Duka
hili si tu litasaidia katika kuongeza mapato kwa klabu lakini pia
litaziba mianya yote ya wale watu wote wasio itakia mema klabu yetu na
kuamua kutengeneza vitu feki vyenye chapa ya Simba, kwakuwa sasa mtu
ukikutwa na bidhaa feki basi mkono wa sheria utakuwa juu yako. Nipende
kuwa sisistiza wanachama, wapenzi na wadau wote wa Simba na soka la
Tanzania kwa ujumla kuwa kwanza tupende vyetu vya nyumani lakini pia
tupende kutumia vitu halisi na kuachana na utamaduni wa mazoea ya
kutojali ni kipi halisi na kipi ni feki” aliongeza Rais Aveva
Akizungumza
kwenye ufunguzi huo Mkurugenzi wa kampuni ya EAG Group Ltd ambao ni
washauri na watekelezaji wa masuala ya biashara na masko kwa klabu ya
Simba Bw. Imani Kajula alisema “nadhani sasa wanasimba tunaweza
kufurahia vya kwetu kwani kwa sasa tunajua ni wapi vinapatikana na ni
wapi ukienda huwezi kukutana na kitu feki chenye chapa ya Simba na hapo
si pengine bali ni Simba Sports Shop lililopo katika jingo la DarFree
Market. Pamoja na kuwepo kwa duka hili lakini pia vifaa vyote
vitakavyokuwa vikipatikana hapa ndani ya siku za hivi karibuni vitakuwa
vikipatikana kwenye duka mtandao (Online Shops) na hivyo kuweza
kuwafikia watu wote popote walipo nchini Tanzania”.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa duka hilo msimamizi wa Duka la vifaa vya michezo venye chapa ya Simba mkurugenzi wa kampuni ya Insight Media Bw. Tahir Othman ambao ni waamiliki wa Dukakwa
kuhamasisha wapenzi wote wa Soka Tanzania kuweza kuunga mkono juhudi
zinazofanywa na klabu ya Simba ili kuweza kukuza mapato kwa klabu yetu
lakini pia kuweza kupata bidhaa bora na halisi za chapa ya Simba.
Post a Comment