Mkuu wa wilaya ya Liwale mh.Ephraim Mmbaga
Serikali kwa shirikiana
na wananchi wa Halmshauri ya wilaya ya
Liwale mkoani Lindi imeungana na kuwahamisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima
ya afya ya jamii (CHF) ili kuweza kupata matibabu kwa mwaka mzima.
Hayo yalisemwa na Ephraim Mmbaga mkuu wa wilaya ya Liwale
ofisini kwake alipotembelewa na waandishi wa habari leo pia waandishi waliweza kuunga mkono wa kampeni hiyo ya
kuchangia mfuko wa bima ya afya ya jamii kwa kulipia kaya 5 zenye makundi
maalumu ambayo thamani yake shilingi elfu hamsini (50000).
Miongoni mwa waandishi wa habari waliochangia familia au kaya
zisizojiweza ni Mwandae Mchungulike mwanmdishi na miliki wa Liwale Blog,Bilingita
Kambona na Anna Milanzi.
Mmbaga alisema mwaka huu wananchi wengi sana wameamasika sana
kujitokeza katika kampeni hii ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii katika
kila kata na kila kijiji baaada ya kufanya kampeni wilaya mzima hii imetokana
na uhamasishaji wa mwaka jana kampeni iliyokuwa ikiitwa KUKU MMOJA MATIBABU KAYA MZIMA.
Kampeni ya kuku mmoja matibabu kaya mzima ikiwa na maana
ukinunua kuku mmoja mdogo kwa elfu kumi bora kuchangia bima ya afya ya
jamii pia alibainisha moja ya tatizo lililokuwa
linawakatisha wananchi ni wakichangia bima ya afya ya jamii alafu wanapokwenda
kwenye vituo vya afya dawa hazipo.
Mkuu wa wilaya aviaziga vyombo vya
uchunguzi kuchunguza kunanini nyumba ya wanaopokea pesa hii pia amwagiza katibu
tawala wilaya Wilson Nyamanga kufuatilia kila senti tano inayochangwa na
wananchi kwa swala la bima ya afya ya jamii alisimia 67 itaenda kwenye kununua dawa
na asilimia 23 itatumika kwa shughuli zingine za uendeshaji na utawala.
“Hakuna wananchi aliyechangia bima ya afya ya jamii
hatakufa kwa kukosa dawa hospitalini” Alisema mkuu wa wilaya.
Mmbaga alisema kama wananchi wa
Liwale aliyechangia akienda hospitali akikosa dawa mtendaji mkuu wa serikali
ataeleza pesa zimeenda wapi.
Pia aliwashukuru waandishi wa habari
waliotembelea ofisini kwake na kuunga mkono kampeni ya kuchangia bima ya afya
ya jamii.
Katibu tawala wilaya Wilson Nyamanga
alisema mpanga huu wa bima ya afya ya jamii ulikuwa mpango shirikishi na
alibainisha kuwa vipo vijiji vilivyojitolea kulipia kaya zote zilizo katika
vijiji vyao baadhi ya vijiji hivyo ni Mirui,Naujombo,Ndapata na pamoja na chama
na chama cha msingi Umoja kilihadi kitawalipia wanachama wake wote 750.
Kuhusu elimu bure katika wilaya ya Liwale mkuu wa wilaya alisema
mwaka huu kuna mlipuko mkubwa sana wa uandishishwaji wa watoto wanaojiunga na
darasa la kwanza na kuna watoto wengine wana umri wa miaka 13 mwaka huu wazazi
wakidai walikuwa wanashindwa kuwapeleka watoto wao kwa kukosa pesa pia waliwaagiza
wakuu wa shule zote kufuatilia mahudhulio ya wanafunzi ya kila siku.
Mmbaga anawaomba wananchi kulima kilimo cha mazao
yanayohimili hali ya hewa na kupanda mazao ya chakula ya muda mfupi ili kuweza
kuondokana na tatizo la njaa.
Mkuu wa wilaya alimpongeza mwandishi wa habari na mmiliki wa
Liwale Blog kwa mchango mkubwa juu ya uhamasishaji wa suala la usafi katika
wilaya ya Liwale.
Post a Comment