Naibu Rais wa Kenya
William Ruto amepata ushindi muhimu kwenye kesi yake inayosikizwa
katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) baada ya majaji wa rufaa
kukubali rufaa yake ya kupinga kutumiwa kwa ushahidi wa mashahidi
waliojiondoa.
Hii ina maana kwamba ushahidi ulioandikishwa awali
na upande wa mashtaka hauwezi kutumiwa dhidi ya Bw Ruto na mwanahabari
Joshua Sang.Uamuzi huo ni pigo kubwa kwa upande wa mashtaka unaoongozwa na Fatou Bensouda.
Upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi sita waliokuwa wanahusisha Bw Ruto na ghasia za baada ya uchaguzi za mwaka 2007-08, vilivyosababisha vifo vya watu 1,200, walioondoa ushahidi wao.
Upande wa mashtaka unasema walitishiwa au wakahongwa.
Majaji wa rufaa wamebatilisha uamuzi wa awali wa majaji uliosema upande wa mashtaka unaweza kutumia ushahidi uliowasilisha na mashahidi hao kabla yao kubadili nia.
"Ushahidi ulioandikisha awali uliwasilishwa bila washtakiwa kupewa fursa ya kuwahoji na kuwauliza maswali mashahidi hao,” amesema jaji wa mahakama ya rufaa Piotr Hofmanski.
Bw Sang amefurahia uamuzi huo na kusema maombi yake yamejibiwa.
Post a Comment