0
 
Maalim Seif na Edward Lowassa
Makamu wa kwanza wa rais wa serikali ya visiwa vya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameishutumu serikali ya Tanzania kwa kufumbia macho makundi yanayowavamia na kuwapiga wafuasi wa chama cha upinzani cha CUF
Mkuu wa polisi kisiwani Zanzibar, Kamishna Hamdan Omar Makame amezikanusha tuhuma hizo na kuhoji kuwa iwapo kuna watu walioshambuliwa ni kwa nini hawajashtaki.
Chama cha CUF kimeendelea kusisitiza kuwa kilishinda katika uchaguzi uliopita na hivyo hakitashiriki katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 20 Machi na serikali iache kufanya hujuma zitakazoivuruga nchi.
Awali Maalim Seif amesema mara kadhaa amefanya juhudi za kuwasiliana na wakuu wa usalama lakini wamemtaka kwanza kupitia kwa Waziri wa nchi aliye katika Ofisi ya makamu wa pili wa Rais jambo ambalo limemshangaza yeye kwani ni kinyume cha protokali Makamu wa Rais kuomba ruhusa kwa Waziri.
Makamu huyo wa Rais anayekiwakilisha chama cha upinzani katika serikali ya visiwa hivyo, amesema ameongea na Rais Shein wa Zanzibar pamoja na makamu wa pili Balozi Seif Ali Idd lakini wote wamesema hawajui lolote kuhusu kundi hilo linalowashambulia wapinzani.
Kundi hilo ambalo limepewa jina la 'Mazombie' kwa mujibu wa Maalim Seif hujifunika nyuso zao kwa soksi nzito ili kukwepa kutambulika.
"Serikali ilitumia mabilioni kufunga kamera za CCTV katika maeneo mengi ya Zanzibar,Matukio ya Ngome Kongwe ambako kumefungwa kamera hawajatuambia iwapo wamemkamata mtu hata mmoja" Amesema Maalim Seif aliyekuwa ameambatana na Edward Lowassa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania lakini akakihana chama chake cha CCM na kuhamia chama cha Upinzani.
Chama cha CUF kimeendelea kusisitiza kuwa kilishinda katika uchaguzi uliopita na hivyo hakitashiriki katika uchaguzi utakaofanyika tarehe 20 Machi na Serikali iache kufanya hujuma zitakazoivuruga nchi.

Post a Comment

 
Top