Sepp Blatter amesema hatomuunga mkono yeyote kati ya wagombea watano wanaosimama katika uchaguzi wa kumrithi kama rais wa FIFA, japokuwa wote isipokuwa mmoa wamezungumza naye kuhusu maombi yao
Na sasa Mswisi huyo anasema wagombea watano wamezungumza naye, lakini hawezi kuegea upande wowote, maana hilo haliwezekani. Aidha amesema mashirika kadhaa ya kitaifa yamemuuliza nani yanapaswa kumpigia kura, lakini akayaambia yapige kura kutokana na uamuzi wao. Blatter anasikitika kuwa vyombo vya habari vilimwangamiza "ninachojutia ni jinsi vyombo vya habari vilivyoamua kuniuwa kuanzia siku ya kwanza. shutuma dhidi ya rais wa FIFA kutoka kwa vyombo vya habari wakati sikuwa mwenye anayewajibikia hatua za wanachama wa Kamati Kuu kwa vile sio mimi ninayewachagua. majuto yangu ni kuwa, labda, kuwa hatuchukua hatua mwafaka ili kuepuka kuwa na wanachama wa kamati kuu ya FIFA ambao hawakupita mtihani wa uadilifu".
Wagombea wakuu wawili ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa wa Bahrain na Katibu Mkuu wa UEFA Gianni Infantino wa Uswisi. Wengine ni Mwanamfalme wa Jordan Ali bin al-Hussein, Mfaransa Jerome Champagne, naibu katibu mkuu wa zamani wa FIFA, na mfanyabiashara wa Afrika Kusini na mwanasiasa Tokyo Sexwale.
Post a Comment