0
kwa upande wa kushoto ni Mratibu wa CHF wilayani Liwale bwana Evarist Malima alikaa katikati Mary Ding’ohi afisa maendeleo ya jamii  na Brigton Makelele mwakilishi wa Wama wilayani Liwale.



Katibu tawala wilaya ya Liwale mkoani Lindi Wilson Nyamanga aitisha kikao leo ofisni kwake kilichohusisha Taasisi mbalimbali na waandishi wa habari kwa lengo la kutafuta utatuzi wa changamoto zilizopo katika jamii.

Akizungumza na Taasasi zisizo za kiserikali ya OlidIngo,viongozi wa vikundi vya vikoba na mratibu wa bima ya afya ya jamii CHF alisema azima ya kuitisha kikao hicho ni kutaka viongozi wa vikundi kuwahamasisha wanachama wao wote wa  vikoba vilivyopo hapa wilayani kuweza kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii ambayo huchangia kiasi cha shilingi 10000 hutibiwa  kaya moja yenye watu 6 na kuifanya kaya hiyo kuweza kutibiwa kipindi cha mwaka mzima.

Kwa upande wake Brigton Makelele mwakilishi wa Wama wilayani Liwale alisema amefurahishwa sana kikao hicho na kufungua ukurasa mpya wa mahusiano pia amebainisha kuwa kunauwezekano mkubwa sasa wa kutembelea vikundi mbalimbali vilivyopo hapa wilayani na kuwahamasisha kuweza kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii kupitia pesa wanazochangishana katika vikundi hivyo ambazo huitwa pesa za tahadhari na kuweza sasa kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii kwa lengo la kujihakikishia kuweza kupata matibabu ya mwaka mzima.

Mratibu wa CHF wilayani Liwale bwana Evarist Malima alisema kila Mtanzania ni vyema akajiunga na bima ya afya kwa kuzingatia kwamba bima hii hakuna masharti magumu katika kujiunga kwake pia ameziomba Asasi mbalimbali kuweza kusaidia kuzilipia kaya zisizojiweza au maskini katika maeneo yao aliongeza kusema hadi sasa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wameweza kuwaunganisha kwenye mfuko huo ni 1260.

Viongozi wengine waliohudhulia kwenye kikao hicho  ni Mary Ding’ohi afisa maendeleo ya jamii  alisema idara yake inafanya kazi na Taasisi mbalimbali zilizilizopo hapa wilaya na kufuatilia kwa ukaribu katika vikundi vyote na popote vilipo bila kuangalia kipo chini ya nani.

Katibu wa  Olidingo ambayo ni NGO’S  bwana Ally Ligai alisema Olidingo ni mratibu wa washughuli zote za vikundi hapa wilayani Liwale na kufanyakazi ya pamoja kwa kufuata kanuni na utaratibu pia alibainisha kuwepo kwa changamoto ya ushirikiano mdogo kwa baadhi ya Taasisi zinazokuja kufanya kazi hapa wilayani bila kushirikiana na Olidingo na kusababisha jamii kukosa kupata taarifa sahihi na aliongeza kusema kupitia kikao hichi wamefungua ukurasa mpya wa ushirikiano katika utendaji kazi.

Katibu tawala akifunga kikao alibainisha kuwa kwa jitihada za viongozi wa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameweza kushawishi kaya zaidi kutoka 2110 na kuongezeka baada ya kufanya kampeni ya kuwashawishi wananchi hadi sasa idadi ya kaya zimeongezeka na kufikia kaya sasa zaidi ya 5000 na wanatarajia kupata ongezeko kubwa zaidi ya hapo, idadi kamili itaelezwa katika kikao cha tathumini kinachotarajia kufanyika mwezi march 2 mwaka huu pia aliongeza kusema  serikali kwa kushirikiana na Taasasi mbalimbali kupitia kikao hiki wameadhimia kuitisha mkutano mkubwa uliopewa jina la jukwaa la wadau wa Liwale.

Post a Comment

 
Top