Rais
Barack Obama alitokwa na machozi jana alipokuwa akitetea kufanyiwa
mabadiliko kwa sheria za udhibiti wa silaha nchini Marekani ili
kupunguza idadi ya watu wanaoshambuliwa na kuuawa kwa risasi nchini
humo.
Obama
aliwaambia Wamarekani kwamba mageuzi anayoyatete ni kwa manufaa yao
wenyewe kwa kuwa yeye huu ni mwaka wake wa mwisho kukaa madarakani na
wala hana mpango wa kugombea tena.
Rais
Obama anataka watu wote wanaouza silaha washurutishwe kuwapekua na
kuchunguza historia ya watu wanaowauzia silaha. Kwa sasa, sheria
hiyo hugusa tu wauzaji silaha waliosajiliwa. Wauza silaha ambao
hawajasajiliwa, hutakiwa kuwauliza tu wateja wao iwapo wamewahi
kupatikana na makosa ya uhalifu au kama wana matatizo ya kiakili.
Hatua
hiyo ya Rais Obama imepingwa vikali na baadhi ya viongozi wakuu wa chama
cha Republican wanaosema inaingilia uhuru wa kikatiba wa Wamarekani.
VIDEO YA OBAMA AKITOKWA NA MACHOZI HII HAPA CHINI
VIDEO YA OBAMA AKITOKWA NA MACHOZI HII HAPA CHINI
Post a Comment