Waziri
wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba akisalimiana na wadau
wakati wa mkutano wake na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika
pamoja na wakulima, Iringa.
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba amewasimamisha kazi
viongozi wa vyama vya msingi vya tumbaku mkoani Iringa wanaotuhumiwa
kushiriki katika ufisadi wa mkopo wa matrekta 9 kupitia mgongo wa vyama
vya msingi vya wakulima wa tumbaku na kujimilikisha wenyewe.
Mwigulu akisalimiana na wadau
Nchemba alifikia hatua hiyo jana baada ya wakulima wa tumbaku kuwalalamikia viongozi wa vyama hivyo kwa kuwatapeli.
Wakulima wa tumbaku wakiwasilisha malalamiko yao kwa Waziri Mwigulu Nchemba.
Matrekta hayo 9 yaliyoleta mzozo vilikopeshwa vyama vya Msingi na benki
ya CRDB kwa manufaa ya wote na wakulima wamekuwa wakitozwa pesa
wanapoyatumia matrekta hayo ili kulipia madeni benki.
Katika utetezi wao, viongozi hao wa vyama walimwambia Waziri kuwa
Matrekta hayo siyo ya vyama bali ni ya kwao ila walikopa kupitia mgongo
wa Vyama vya msingi vya ushirika.
Mkutano ukiendelea.
Waziri Nchemba aliwahoji viongozi hao kama kuna kiongozi aliyelipia
mkopo wa matrekta hayo kwa fedha yake ambapo wote walisema hawajalipia
ila wamelipiwa na wanachama lakini walipanga yatakuwa ya kwao kwa kuwa
wao ndio wanaosimamia ukusanyaji wa fedha za wanachama kuyalipia
Matrekta hayo.
Utetezi huo ulimtia kichefuchefu Waziri Nchemba na kuamua kuwafukuza kazi viongozi hao na kuamuru benki ya CRDB waandike kadi za matrekta hayo kwa umiliki wa vyama vya Msingi.
Post a Comment