0


Baada ya klabu ya Real Madrid kutangaza rasmi kumfuta kazi aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Rafael Benitez. Real Madrid walitangaza kumfuta kazi Benitez na Zidane kutajwa kurithi nafasi hiyo kwa muda hadi mwisho wa msimu.
Zidane na Beckam
Mchezaji mwenzake wa zamani David Beckham hakuweza kuficha kuonesha furaha yake kwa kupost picha yao ya zamani na ujumbe wenye kuoneshwa kufurahishwa na nguli huyo wa kifaransa kuchukua mikoba hiyoo.
“Unaweza kumpata mtu bora zaidi yake? mtu ambaye alikuwa bora kiwanjani na watu wote tunampenda, anachukua nafasi ya kutumikia klabu ambayo mimi na watu wengine tunaipenda, mtu mwenye passion na siku zote huwa hakubali kushindwa kwa namna yoyote ile. Kiukweli ni mtu sahihi kwa hiyo kazi”>> Beckham

Beckam na Zidane

Post a Comment

 
Top