0

Uongozi wa klabu ya Real Madrid hatimaye umemfukuza kocha wake Rafael Benitez ambaye amedumu kwa miezi 7 pekee.
Nafasi ya Benitez imechukuliwa na aliyekuwa mchezaji wa Ufaransa Zinedine Zidane ambaye awali alikuwa kocha wa kikosi B cha Real Madrid.
Hii ni kutokana na matokeo mabaya kwa timu hiyo, ambapo ilitoka sare 2-2 na Valencia, katika Mechi ya La Liga, sare ambayo imewaacha vigogo hao nafasi ya 3 wakiwa nyuma ya Atletico Madrid kwa pointi 4.

Tangu atue Madrid, Benitez amekuwa hapendwi na mashabiki wa klabu hiyo, baada ya kufungwa bao 4-0 kwenye mechi ya El Clasico mwezi Novemba na mahasimu wao Barcelona, pia kutupwa nje ya michuano ya Copa del Rey.

Post a Comment

 
Top