Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na
klabu ya Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ameamua kustaafu kuichezea timu
hiyo ili kuweka nguvu kwenye klabu yake Yanga
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na klabu ya Yanga
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ameamua kustaafu kuichezea timu hiyo ili kuweka
nguvu kwenye klabu yake ambayo inapambana kutetea ubingwa wa ligi ya
Vodacom Tanzania bara.Cannavaro ameiambia Goal yapo mambo mengi yaliyomfanya ajiondoe kuichezea timu hiyo moja wapo ni kitendo kilichofanywa na kocha mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwassa kumteua mshambuliaji Mbwana Samatta kuwa nahodha bila kumpa taarifa kabla na kingine ni lawama anazopata kutoka kwa mashabiki ambao wanadai yeye ndiye anayeifungisha timu hiyo.
“Nimecheza kwa miaka 10, mengi nimefanya na nimepata acha niwaachie wengine waje kuichezea Stars kwa mafanikio makubwa katika kuhakikisha inapata mafanikio katika siku za baadaye.
“Naamini ni maamuzi sahihi kwa wakati sahihi kwangu kutangaza kustaafu kuichezea Stars, ninaamini wapo wachezaji wengi wanaochipukia watakaonirithi mimi na wakongwe wenzangu,” anasema Cannavaro.
Cannavaro anasema maneno yamekuwa mengi na yalianza mara baada ya mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Algeria kule kwao.
“Katika mechi hiyo tulifungwa mabao 7-0, mechi hiyo muda mwingi tulicheza pungufu baada ya Mudathiri (Yahya) kutolewa kwa kadi nyekundu, tulijitahidi kupambana kuhakikisha tunawatoa Algeria lakini ikashindikana, cha ajabu mara baada ya mechi hiyo nilionekana mimi pekee ndiye niliyefungisha, nilijisikia vibaya sababu nilipambana kwa ajili ya taifa langu na mwisho wa siku naonekana si lolote,”anasema Canaavaro.
Baada ya kusikia hayo maneno na kocha kumtangaza Samanatta kama nahodha mpya ameona nibora ajiweke pembeni na amepanga kupeleka barua rasmi kwa Shirikisho la TFF ya kuwapa taarifa ya kustaafu kwake kuichezea timu ya taifa.
“Nguvu zangu zote nitazihamishia katika klabu yangu ya Yanga. Hivi sasa nimepona majeraha ya enka niliyoyapata nikiwa naitumikia Stars tulipocheza na Algeria, hivyo ninaamini baada ya wiki mbili nitarejea uwanjani,” anahitimisha Cannavaro.
Post a Comment