Rais wa Burkina
Faso amesema takriban watu 21 wameuwawa katika shambulio kwenye hoteli
moja mjini Ogadugu na wanamgambo waliovamia hotel hiyo.
Roch Mark
Christian Kabore amesema washambuliaji wanne waliovamia hotel hiyo
waliuliwa ambapo wawili kati yao ni wanawake. Shambulio hilo lililotokea
kwenye hotel ya Splendide kwenye mji mkuu wa Ouagadougou sasa
limemalizwa.Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo amesema wanamgambo hao wameuwa watu kumi na nane kutoka mataifa mbalimbali. Zaidi ya watu mia moja na ishirini walikimbia hotel hiyo maarufu kwa watalii.
walionusurika wanasema wanamgambo hao walianza kupiga risasi kwenye jengo hilo na kisha kuliwasha moto.
Kundi la Kigaidi la Al Qaeda kwenye ukingo eneo jangwa imesema lina husika na shambulio hilo.
Watu 126 waliokuwa mateka waliachiliwa huru katika hoteli ya Splendid iliopo katika mji mkuu wa taifa hilo la Magharibi mwa Afrika Ouagadougou, kwa mujibu wa waziri wa maswala ya ndani.
Wapiganaji wanne waliuawa aliongezea huku watu 21 wa mataifa 18 tofauti wakifariki wakati wa shambulio ambalo pia liliulenga mgahawa huo.
Vikosi maalum vya Ufaransa vinasaidia wanajeshi wa taifa hilo katika oparesheni hiyo.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameshtumu shambulio hilo la taifa hilo ambalo lilikuwa koloni yake hapo zamani.
Kundi la Al-Qaeda la islamic Maghreb{AQIM} limesema kuwa lilitekeleza shambulio hilo katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika.
Mnamo mwezi Novemba shambulio la AQIM katika hoteli moja ya Bamako nchini Mali liliwauwa watu 19.
Post a Comment