Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Revocatus Malimi.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Revocatus Malimi, alisema
jana kuwa tukio hilo limetokea juzi saa sita mchana katika mji mdogo wa
Peramiho, nje kidogo ya Manispaa ya Songea.
Malimi alisema inadaiwa kuwa siku hiyo ya tukio, Mwalimu Mkuu
Msaidizi, Rashid Pilly, aligundua kujinyonga kwa mwalimu huyo, baada ya
kupita eneo la nyumba aliyokuwa anaishi na kuona nzi wengi wametapakaa
kwenye eneo la dirisha la chumba alichokuwa analala.
Alifafanua zaidi kuwa Mwalimu Pilly baada ya kuona hali hiyo,
alisogea hadi mlangoni na kukutwa mlango ukiwa umefungwa huku eneo hilo
likiwa na harufu kali iliyoashiria kuna kitu ambacho kimeoza.
Alisema baadaye Mwalimu Pilly alilazimika kwenda kutoa taarifa
kwenye kituo kidogo cha Polisi cha Peramiho na baadaye askari polisi
wakiwa wameongozana na mganga, walifika eneo la tukio.
Baada ya kufika, alisema walivunja mlango na kuingia ndani ya
nyumba hiyo ambako walimkuta Mwalimu Mwakajila akiwa tayari ameshakufa
muda mrefu baada ya kujinyonga.
Alisema Mwakajila alijinyonga ndani ya nyumba ambayo ni mali ya
shule na askari walikuta barua chini ya sehemu aliyojinyongea iliyokuwa
imeandikwa Januari 4 mwaka huu na mwanamke (jina linahifadhiwa),
anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, ambaye alimtaka aachane naye na aendelee
na maisha yake.
Malimi alisema polisi baada ya kuiona na kuisoma, waliendelea
kuufanyia upekuzi mwili wa marehemu na kukuta pia karatasi kwenye mfuko
wa suruali yake, ambayo Mwakajila aliandika Januari 2, mwaka huu,
akimtuhumu mpenzi wake huyo kuwa amekuwa malaya na mlevi
Kamanda Malimi alisema polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi
kuhusiana na tukio hilo na mwili wa marehemu umekabidhiwa kwa ndugu kwa
ajiki ya taratibu za mazishi.
CHANZO:NIPASHE
Post a Comment