Mahakama
Kuu Kanda ya Mwanza leo imeanza kusikiliza Kesi ya Kupinga Matokeo ya
uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana katika Jimbo la Bunda
Mjini, Mkoani Mara ambapo Mgombea kutoka Chama cha Demokrasia na
Maendeleo Chadema Esther Bulaya aliibuka mshindi.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Jaji
wa Mahakama hiyo Mhe.Mohamed Gwae ameahirisha kesi hiyo hadi jumatatu
ijayo ya Januari 25 mwaka huu baada ya mawakili wa pande zote mbili
kuchuana vikali kwa muda mrefu.
Waleta
maombi (Mlalamikaji) katika kesi hiyo wametajwa kuwa ni wapiga kura wa
jimbo hilo la Bunda Mjini ambao walikuwa wakiiomba Mahakama kutengua
matokeo ya uchaguzi huo katika jimbo hilo kutokana na uchaguzi huo
kukumbwa na kasoro mbalimbali ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru pamoja na
idadi ya wapiga kura kutofautiana na idadi ya waliojiandikisha katika
daftari la kudumu la wapiga kura.
Madai
hayo yamepingwa na upande wa Mjibu Maombi (Walalamikiwa ambao ni Mbunge
wa Jimbo la Bunda Mjini pamoja na Mwanzasheria wa Serikali) uliokuwa
ukiongozwa na Wakili Tundu Lisu. Upande wa Mleta maombi ulikuwa
ukiongozwa na Wakili Constantine Mutalemwa.
Kesi
hiyo ilianza kusikilizwa majira ya saa tatu asubuhi na baadae
kuahilishwa kwa ajili ya chakula cha mchana na kisha kuendelea
kusikilizwa kuanzia majira ya saa nane mchana hadi majira ya saa kumi na
moja jioni.
Wakili
upande wa mjibu maombi Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza baada ya
Kesi hiyo kuahirishwa ambapo amesema hoja za waleta maombi hazina
mashiko kwani katika hati yao ya madai hawajalalamika kuonesha kama haki
yao imekiukwa hivyo ni vyema mahakama ikatupilia mbali maombi yao kwani
yanaonyesha kuwa yanampigania Steven Wasira (aliekuwa mgombea ubunge
kutoka CCM Steven Wasira) ambae hata hivyo hakuwemo mahakamani hapo.
Wakili Tundu Lisu (mwenye miwani) akizungumza baada ya Kesi hiyo kuahirishwa
Wakili
upande wa mleta maombi, Constantine Mutalemwa (mwenye miwani)
akizungumza baada ya kesi hiyo kuahilishwa ambapo amesema kuwa waleta
maombi wanasubiri maamuzi yatakayotolewa na mahakama hiyo baada ya hii
leo kuahirishwa.
Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya (Chadema).
Post a Comment