0
 
Mwanajeshi akikabiliana na wavamizi wa hoteli ya Splendid nchini Burkina Faso
Oparesheni ya kuizunguka hoteli moja iliovamiwa na wapiganaji imeisha ,serikali imetangaza,lakini ripoti zinaarifu kwamba hoteli nyengine iliopo karibu imeshambuliwa.
Watu 126 waliokuwa mateka waliachiliwa huru katika hoteli ya Splendid iliopo katika mji mkuu wa taifa hilo la Magharibi mwa Afrika Ouagadougou, kwa mujibu wa waziri wa maswala ya ndani.
 
Magari ya kijeshi yakipiga doria nje ya hoteli ya Splendid
Wapiganaji watatu waliuawa aliongezea huku kukiwa na ripoti kwamba watu 20 walifariki wakati wa shambulio ambalo pia liliulenga mgahawa huo.
Vikosi maalum vya Ufaransa vinasaidia wanajeshi wa taifa hilo katika oparesheni hiyo.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameshtumu shambulio hilo la taifa hilo ambalo lilikuwa koloni yake hapo zamani.
 
Hali ya kawaida yarudi Burkina Faso
Kundi la Al-Qaeda la islamic Maghreb{AQIM} limesema kuwa lilitekeleza shambulio hilo katika taifa hilo la Magharibi mwa Afrika.
Mnamo mwezi Novemba shambulio la AQIM katika hoteli moja ya Bamako nchini Mali liliwauwa watu 19.

Post a Comment

 
Top