Mfungwa kwenye
gereza la Guantanano Bay ambaye alipinga kufungwa kwake kwaakususi
chakula kwa muda mrefu amechukua hatua isiyo ya kawaida kwa kukataa
kundoka gereza hilo la Marekai nchini Cuba, alipokataa kupelekwa nchi
mpya asiyoifahamu
Muhammad Bawazir, raia wa Yemen mwenye umri wa
miaka 35 alikataa kuabiri ndege kama wafungwa wengine wawili waliokuwa
wakisafirishwa kwenda mataifa ya Balkans kwa mjibu wa wakili wake.Kutoka na sababu hangepelekwa kwao nyumbani , alisisitiza kupelekwa nchi ambapo kuna familia yake.
Wakili wake alilimbia shirika la habari la AP kuwa imechukua miezi kadha kumshawishi Bawazir kukubali kupelekwa nchi nyingine ambayo hakuitaja.
Lakini mfungwa huyo ambaye alikuwa na miaka 21 wakati alikamatwa nchini Afghanistan alikataa dakika za mwisho kuwa hangefanya hivyo.
Post a Comment