0
Korea Kaskazini imesema imefanikiwa kufanya jaribio la bomu la haidrojini. Jaribio hilo limezua hofu nchini Japan na Korea Kusini huku jumuiya ya kimataifa ikilaani hatua hiyo ya Korea Kaskazini.
Jaribio hilo, lililofanywa leo na Korea Kaskazini, taifa ambalo limetengwa na Jumuiya ya kimataifa, limeagizwa kufanywa na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un.
Kituo cha televisheni cha serikali ya Korea Kaskazini kimeonyesha waraka ulioandikwa na Kim ukisema wacha ulimwengu uitizame nchi imara na inayojitegemea kwa kujihami na silaha za kinyuklia.
China ambayo ni mshirika wa Korea Kaskazini imelaani jaribio hilo la bomu la kutumia gesi ya haidrogeni na kusema itawasilisha malalamiko yake kwa nchi hiyo.
Bomu la Haidrogini lina nguvu zaidi
Licha ya kuwa jaribio la nne la kinyuklia lilikuwa linatarajiwa kufanywa na nchi hiyo, madai ya kuwa ni bomu hilo ambalo lina nguvu zaidi ya bomu la atomiki, halikutarajiwa kufanyiwa majaribio.
Kituo cha Televisheni cha Korea Kaskazini kikiripoti jaribio la bomu Kituo cha Televisheni cha Korea Kaskazini kikiripoti jaribio la bomu
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa litafanya mkutano wa dharura leo mjini New York kujadili hatua hiyo ya Korea Kaskazini. Mkutano huo wa faragha umeitishwa na Umoja wa Mataifa na Japan.
Msemaji wa Marekani, Hagar Chemali, amesema hawajaweza kuthibitisha iwapo ni kweli jaribio hilo la bomu limefanywa na wanalaani ukiukaji wowote wa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuitaka Korea Kaskazini kuheshimu wajibu wake wa Kimataifa.KUENDELEA KUSOMA BOFYA HAPA

Post a Comment

 
Top