0
 
Rais Buhari aliahidi kupambana na ufisadi
Wanasiasa nchini Nigeria wanadaiwa kuiba dola billioni 6.7 pesa za umma katika kipindi cha miaka saba kwa mujibu wa waziri wa habari Lai Mojammed.
Magavana, mawaziri, wafanyibiashara, maafisa wa serikali , wafanyikazi wa benki wote wao waliiba pesa hizo kati ya mwaka 2006 na 2013.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari alichaguliwa mwezi machi mwaka uliopita alipoahidi kuwa atapambana na ufisadi.
Alikuwa amemlaumu mtangulizi wake Goodluck Jonathan kwa kufumbia macho wizi wa pesa ambapo aliahidi kurejesha nchini humo pesa zote za umma zilizoibiwa.
Maafisa wa vyeo vya juu katika serikali ya bwana Jonathan wamekamatwa kwa kuiba dola bilioni mbili zilizonuiwa kununua silaha kilipiga vita kundi la Boko Haram.

Post a Comment

 
Top