Iran imepuuzilia mbali vikwazo vipya dhidi yake ilivyowekewa na Marekani kuhusu mpango wake wa kutengeza makombora.
Vikwazo hivyo havina 'uhalali wa kisheria wala wa kimaadili',msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni amesema.Mnamo mwezi Oktoba ,Iran ililifanyia jaribio kombora lake lililo na uwezo wa kubeba kichwa cha kombora la nuklia,ikikiuka marufuku ya Umoja wa mataifa.
Vikwazo hivyo vipya vitawazuia watu na makampuni 11 wanaohusishwa na mpango huo wa kutengeza makombora kutotumia mfumo wa benki wa Marekani.
Hatahivyo msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Iran Hossein Jaber Ansari amesema kwamba mpango huo wa kutengeza makombora haujatengezwa kuwa na malengo ya kubeba silaha za kinuklia.
Post a Comment