Guinea ilifunga
katika muda wa lala salama na kupata droo ya 2-2 dhidi ya Tunisia katika
mechi ya kundi Cha katika mashindano ya soka barani Afrika miongoni mwa
wachezaji wanaosakata soka barani.
Ahmed Akaichi wa Tunisia alifunga bao la kwanza jana katika dakika ya 32 mda mfupi baada ya kombora lake kupiga mlingoti wa goli.Hatahivyo Alseny Kamara aligusa pasi nzuri na kusawazisha kunako dakika 39,lakini baada ya muda wa mapumziko Akaichi aliimarisha azma ya Tunisia alipofunga bao la pili.
Guinea ilinusurika baada ya kichwa cha Zied Boughatt kupiga mlinghoti wa goli kabla ya Tunisia kupata bao la kusawazisha wakati Camara alipofunga bao la pili kutoka kwa kona.
Huku pointi hiyo ikishabikiwa na Guinea,mashabiki watakuwa na wasiwasi baada ya Camara kubebwa na kutolewa nje ikiwa imesalia dakika 3 na watatumai kwamba yuko vyema ili kuweza kuendelea na mechi hizo.
Post a Comment