Na Ezekiel Kamanga, Mbozi
MAHAKAMA ya mwanzo vwawa mjini wilayani Mbozi mkoani Mbeya imemuhukumu Patrick Moses(19) mkazi wa Ilembo kutumikia jela miaka mitano baada ya kukiri kosa la kuiba Mbuzi mmoja mwenye thamanai ya Sh 85,000 mali ya Bahati Mtafya.
Akisoma
hukumu hiyo hakimu wa mahakama hiyo,lazima Mwaijega alisema kutokana
kifungu cha sheria 268 na mshitakiwa kukiri kosa hivyo mahakama imeamuru
mshitakiwa kutumikia kifungo hicho ili iwe fundisho kwake na kwa
wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo.
Mshitakiwa
alipopewa nafasi ya kujitetea aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwani
anategemewa na familia yake,hata hivyo hakimu Mwaijega amesema kifungo
hicho cha miaka mitano amepunguziwa pia kwa kuwa ni kosa lake la kwanza
na kwamba.
Awali imeelezwa mahakamani na mwendesha mashitaka wa polisi Hamis Mohamed kuwa January 20,mwaka huu saa 11 jioni mshitakiwa
alivamia nyumbani kwa Bahati Mtafya (38) na kuiba mbuzi mmoja mwenye
thamani ya Sh. 85,000 huku akijua kufanya vyo ni kosa kisheria namba 229
sura ya 16 kanuni ya adhabu.
Aidha
mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa
mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa wale wenye nia ya kutendakosa
kama hilo kutokana na wimbi kubwa la vijana kujikita katika wizi na
kuacha kufanya kazi halali.
Katika hatua
nyingine mshitakiwa huyo alipandishwa kizimbani hapo kujibu tuhuma ya
wizi wa kuku 23 wenye thamani ya Sh laki 4 mali ya Evance Mwakenja mkazi
wa Ilembo Vwawa
Imeelezwa
mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa polisi Hamis Mohamed kuwa
tukio hilo lilitokea januari 20 mwaka huu saa 8 usiku ambapo mshitakiwa
aliiba kuku 23 wenye dhamani ya Sh.laki 4 mali ya Evance Mwakenja huku
akijua kufanya hivyo nikosa kisheria.
Hata hivyo
mshitakiwa alikana shitaka linalomkabili na hakimuwa mahakama hiyo
Chirstina Mlwilo amesema shauli hilo litaanza kusikilizwa Januari 27
mwaka huu,pia hakimu huyo amesema dhamana kwa mshitakiwa ipo wazi kwa
ahadi ya Sh.laki 4 pamoja na kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya mpiga kura.
Hata hivyo mshitakiwa ameludiswa maabusu kwa kushindwa kutimiza masharti la dhamana pamoja na kuanza kutumikia kifungo cha miaka mitano ya wizi wa mbuzi.
mwisho.
JAMIIMOJABLOG
Post a Comment