Polisi nchini
Marekani imesema takriban watu 14 wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa
baada ya kupigwa risasi na watu wenye silaha katika mji wa San Bernadino
mashariki mwa Los Angeles.
Watu hao wenye silaha wanasemakana walivalia kijeshi na walitumia silaha za masafa marefu.
Mkuu wa kituo hicho cha watu wenye ulemavu palipoteka mauaji hayo ya kinyama anasema milio ya risasi ilisikika katika jengo lililokodishwa kwa ajili ya hafla iliyoandaliwa na Idara ya Afya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la kijasusi la FBI David Bowdich anasema sababu kubwa ya mauaji hadi haijafahamika.
"Kwa wakati huu ninaelewa moja ya maswali yenu ni kuhusu tukio hili la kigaidi. Ninawaeleza sasa kuwa hatujui kama hili ni tukio la kigaidi kwa hiyo tunaanzia mwanzo kufanya kazi na wenzetu waliopo katika eneo hili. Tunadhani inaweza kuwa, pia inaweza isiwe lakini tunafanya kazi bega kwa bega nao kuanzia mwanzo. Kama mambo yatabadilika tupo hapa na hakuna hatua yoyote itakayopotea wakati uchunguzi utakapokuwa unaendelea." Alisema
Post a Comment