Wakizungumza na ITV katika daraja hilo ambalo linaonyesha
kutoimarishwa kiujenzi wananchi hao wamesema kuwa, kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha wilayani humo, zinaweza kuliondoa kabisa na
matokeo yake ni kusababisha madhara makubwa yakiwemo ya vifo vya
wagonjwa.
Akizungumzia daraja hili diwani wa kata hiyo Bw, Anthony Simon
Makani amesema kuwa, wananchi wanategemea huduma mbalimbali za kijamii
kupitia daraja hilo, hivyo serikali ingewaangalia kimsaada zaidi ili
kuliimarisha kwa lengo la kuwanusuru na majanga ambayo yanaweza
kusababishwa na daraja hilo.
Post a Comment