Winga wa klabu ya soka ya Leicester City na timu ya taifa ya Algeria Riyad Mahrez amesema hana mpango wowote wa kuihama klabu yake hiyo mwezi Januari katika dirisha dogo la usajili, kauli ambayo imesisitizwa pia na kocha wake Claudio Ranieri kuwa wachezaji wake Riyad Mahrez na Jamie Vardy hawauzwi kwa bei yeyote.
Klabu za Arsenal, Manchester United na Barcelona zinamuwania winga huyo aliyesajiliwa kutoka Le Havre ya Ufaransa (daraja la pili) kwa ada ya pauni 400,000 tu mwaka jana 2014 na sasa anataka kuwalipa fadhila Leicester.
Mahrez anasema alipokua Le Havre Ufaransa hakuna klabu yeyote iliyomfuata, zaidi ya Leicester ambapo anasema ilikua ni ngumu kwake kuondoka sehemu aliyoizoea na kwenda England ambapo alikua ni mgeni lakini anawashukuru sana Leicester kwani anafurahia maisha na kwamba lazima abakie hapo kuwalipa fadhila zao.
Kuhusu uhusiano na kocha wake Claudio Ranieri, winga huyo mwenye goli 11 hadi sasa huku akiwa wa pili kwa assists nyuma ya Mesut Ozil wa Arsenal, anasema Ranieri ni kocha mzuri sana, anawatia moyo, wanacheka pamoja mazoezini, anawapa motisha na mbinu nzuri za ushindi uwanjani.
Mahrez akizungumzia maisha ya Ufaransa na sasa nchini England, anasema ligi kuu England ni ngumu na bora zaidi kutokana na ushindani, huku akikiri kujituma zaidi mazoezini na binafsi kama siri ya kipaji chake hivi sasa.
Post a Comment