Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NMB Plc Ineke Bussemaker akizungumza na waandishi
wa Habari kuhusu mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za mikopo
uliozinduliwa na Benki hiyo. Mfumo huo utatutumika kwenye kanzi data ya
Mikopo ya Benki hiyo ( CRB’s) kwa lengo la kuwawezesha wateja wakubwa na
wadogo wa wanaoomba mikopo kuipata ndani ya siku 1 hadi 4 .
Afisa
Mkuu Udhibiti wa Hasara wa Benki ya NMB Bw. Tom Borghols (wa pili
kutoka kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari (hawapo
pichani) namna Benki ya NMB inavyoongoza katika utoaji wa mikopo kwa
makundi mbalimbali.
Kaimu
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB Bw. Abbdulmajid Nsekela(
kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu kuanzishwa kwa mfumo wa kisasa wa
utunzaji wa taarifa za mikopo kwa wateja uliozinduliwa na Benki ya NMB
na jinsi utakavyoongeza ufanisi kwa kuwawezesha wateja kupata mikopo kwa
haraka. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc Ineke
Bussemaker. (Picha na Aron Msigwa).
Na Aron Msigwa – MAELEZO
Benki
ya NMB imezindua mfumo wa kisasa wa utunzaji wa taarifa za wateja
utakaotumika kwenye kanzi data ya Mikopo ya Benki hiyo ( CRB’s) kwa
lengo la kuwawezesha wateja wakubwa na wadogo wa wanaoomba mikopo
kuipata ndani ya siku 1 hadi 4 tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
Akizungumza
na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salam Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya NMB Plc Ineke Bussemaker amesema kuwa utaiwezesha Benki hiyo
kuwahudumia wateja wake katika matawi zaidi ya 170 yaliyoko nchi nzima
kwa haraka zaidi tofauti na kuiwezesha Benki hiyo kuwasiliana na benki
nyingine kwa njia ya mtandao.
”
NMB tumekuwa tukiboresha mifumo yetu ya utoaji wa huduma ili kuwapatia
wateja wetu huduma bora, kulingana na utendaji wa mfumo huu mteja wetu
sasa atapata mkopo wake ndani ya siku 1 hadi 4 tofauti na ilivyokuwa
hapo nyuma ambapo ilichukua takribani wiki mbili mteja kupata mkopo
wake” Amesisitiza.
Amesema
kuwa Benki hiyo husshughulikia maombi ya mikopo zaidi ya 700 kwa siku
na kuongeza kuwa kupitia mfumo huo wa kisasa taarifa za huduma ya utoaji
wa mikopo ndani ya NMB, mishahara ya wafanyakazi inayopitia Benki hiyo,
waombaji wadogo na Wakubwa wa mikopo hiyo ikiwemo wafanyabiashara na
makampuni zitadhibitiwa kutokana na uwepo wa mifumo huo wenye uwezo wa
kuchambua na kuweka kumbukumbu za wateja wanaoomba na kurejesha mikopo
kwa haraka.
Aidha amesema kupitia matumizi ya Mfumo huo ( Simbuka) Benki ya NMB itaweza kufuatiliaji taarifa za wateja kwa ukaribu zaidi.
Kwa
Upande wake Afisa Mkuu Udhibiti wa Hasara wa Benki ya NMB Bw. Tom
Borghols amesema kuwa Benki ya NMB inaongoza katika utoaji wa mikopo
kwa makundi mbalimbali nchini kwa mikopo inayofikia shilingi Trilioni
2.2 kwa mwaka ambapo asilimia 25 ni mikopo midogo na asilimia 25 ni
mikopo kwa wateja wakubwa.
Akitoa
ufafanuzi kuhusu madai ya kiwango cha riba kinachotolewa na Benki za
Tanzania kuwa kikubwa ameeleza kuwa kiwango hicho kinachangiwa na hali
ukuaji wa uchumi wa eneo husika pamoja na gharama za kupata amana za
mikopo na kutoa wito kwa mabenki kote nchini kufanya kazi kwa pamoja ili
kuimarisha utoaji wa huduma za kibenki nchini.
Kaimu
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa Benki ya NMB Bw. Abbdulmajid Nsekela
akitoa ufafanuzi kuhusu kuanzishwa kwa mfumo huo amesema umejengwa kwa
ushirikiano na wataalam kutoka Nethaland,unawezesha ushirikiano wa
taarifa za kibenki kutoka benki moja kwenda nyingine na sasa wateja
watapata mikopo yao ndani ya siku 4 kutokana na taarifa za mifumo
kuwasiliana.
Aidha,
amesema mabadiliko hayo yameanzishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT)
yamechukuliwa kwa umakini na Benki hiyo kutokana na idadi kubwa ya
mikopo na wateja inaowahudumia.
Aidha, amesema kuwa mtandao huo utasaidia Benki ya NMB kufuatilia na kubainisha mwenendo wa wateja wanaolipa vizuri na vibaya..
Post a Comment