Wagombea wa
Republican waWagombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani
wamejibizana kuhusu njia bora zaidi za kudumisha usalama wa taifa na
kukabiliana na Islamic State (IS) kwenye mdahalo wa kwanza tangu kutokea
kwa mashambulio ya California na Paris. Mgawanyiko mkubwa umetokea
kati ya wale wanaotetea kuwepo kwa upeelezi zaidi na wale wanaotetea
haki za kiraia.
Mgombea anayeongoza, Donald Trump, amelazimika kujitetea kutokana na pendekezo lake kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.Mgombea mmoja anayempinga vikali, Jeb Bush, amemwita “mgombea wa vurugu”.
Seneta Marco Rubio na Ted Cruz pia wametofautiana kuhusu juhudi za serikali kupeleleza raia wake.
“Hatuzungumzi kuhusu kutengwa kwa watu, tunazungumzia usalama,” amejitetea Bw Trump. “Hatuzungumzi kuhusu dini, tunazungumza kuhusu usalama.”
- Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na Saddam
- Mambo 20 makuu anayoamini Donald Trump
- Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislamu
Pendekezo jingine la Trump, la kufunga mtandao wa intaneti kuzuia IS kuandikisha wanachama, umejadiliwa sana huku mfanyabiashara huyo tajiri akizomewa alipojaribu kujitetea.
Bw Trump ameonekana kukanganyikiwa na hisia za umati, akisema: “hawa ni watu wanaotaka kutuua jameni.”
Post a Comment