Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Ally Simba
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na
makampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Airtel, Halotel na Zantel na
Smart kwa kuto kukidhi vigenzo. Pia amesema kuwa Makampuni hayo
yamepigwa faini ya shilingi milioni 25 kwa mamlaka ya mawasiliano
Tanzania kabla ya Januari 29 mwakani.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
JAMHURI YA YA MUUNGANO YA TANZANIA
Mwanasheria
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Elizabeth Zagi akifafanua
jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Ally Simba jijini Dar es Salaam leo.Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
JAMHURI YA YA MUUNGANO YA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
HATUA
ZA KISHERIA NA KIUDHIBITI KWA MAKAMPUNI YA SIMU YALIYOSHINDWA KULINDA
WATEJA WAKE KITEKNOLOJIA NA KISHERIA KUHAKIKISHA USALAMA WA MAWASILIANO
YAO
1.
Katika shughuili zake za udhibiti wa huduma za mawasiliano nchini,
Mamlaka ya Mawasilaino Tanzania imepokea malalamiko kutoka kwa watumiaji
wa huduma za mawasiliano dhidi ya kuwepo mazingira yasiyo salama katika
huduma za mawasiliano na hivyo kusababisha kufanyika kwa vitendo vya
utapeli unaofanywa kwa kutuma jumbe za udanganyifu na kulaghai, hivyo
kusababisha watu kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu. Kwa mfano
kupokea ujumbe kutoka namba unayoifahamu ukikuagiza utume fedha au
ujumbe wa kashfa au matusi wakati hautoki kwa mhusika mwenye namba.
Mamlaka imepokea malalamiko mengi kutoka kwa wateja na malalamiko
mengine hupelekwa Polisi. Kwa miezi miwili tu, matukio 42 yameripotiwa
Polisi pamoja na TCRA ambayo tukio moja tu linakuwa na ulaghai wa
takribani milioni 25 peke yake.
2.
Tarehe 16 Oktoba, 2015 Mamlaka iliwakumbusha watoa huduma za simu
nchini juu ya wajibu wao kuchukua hatua za kusheria na kitaalamu ili
kulinda watumiaji dhidi ya utumaji wa jumbe za kilaghai na kuchukua
hatua mara moja kuzuia mitandao yao kutumika kutuma jumbe za udanganyifu
na kulaghai. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na Mamlaka tarehe 16
Desemba, 2015 Mamlaka ilibaini kuwa kampuni za Benson Informatics
Limited (inayojulikana kama Smart), MIC Tanzania Limited (inayojulikana
kama Tigo), Airtel Tanzania Limited, Viettel Tanzania Limited
(inayojulikana kama Halotel) and Zanzibar Telecom Limited inayojulikana
kama Zantel) zimeshindwa, zimepuuzia na zimekataa kufuata maagizo ya
Mamlaka kuchukua hatua mara moja kuzuia mitandao yao kutumika kutuma
jumbe za kilaghai kinyume na Kanuni Na.8(a) ya Kanuni za Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta ya mwaka 2011 [the Electronic and Postal
Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011].
3.
Tarehe 18 Disemba, 2015 Mamlaka iliwaamuru watoa huduma za mawasiliano
waliotajwa hapo juu kufika mbele ya Mamlaka na kujieleza kwa nini hatua
za kisheria zisichukuliwe dhidi yao kwa kuvunja sheria na kanuni ya 8(a)
ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielectroniki na Postal ya Mwaka 2011 [the
Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team)
Regulations, 2011] kwa kushindwa kuweka mazingira salama kwa watumiaji
wa huduma za mawasiliano.
4. Watoa huduma walifika na kutoa maelezo ya utetezi kati ya tarehe 21 na 23 Desemba, 2015.
5.
Baada ya kuwasikiliza na kutilia maanani utetezi wa watoa huduma na kwa
mujibu wa uchunguzi na majaribio uliofanywa na Mamlaka, Mamlaka
imejiridhisha kuwa mitandao ya watoa huduma waliotajwa hapo juu haikuwa
salama na kuwa watoa huduma hao walishindwa kufuata maelekezo ya Mamlaka
juu ya kuweka mazingira salama katika huduma wanazotoa. Hivyo Mamlaka
imejiridhisha kuwa watoa huduma wamekiuka matakwa ya Kanuni ya 8(a) ya
Kanuni za Mawasiliano ya Kielectroniki na Postal ya mwaka 2011 (The
Electronic and Postal Communications (Computer Emergency Response Team)
Regulations, 2011) inayowataka watoa huduma kuweka mazingira ya mitandao
salama kwa kuchukua hatua za kusheria na kitaalamu ili kulinda
watumiaji dhidi ya uhalifu ikiwa ni pamoja na utumaji wa jumbe za
kilaghai kupitia mitandao yao.
6.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 17 cha Jedwali la Pili katika Sheria ya
Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta, Sura ya 306 ya Sheria za Nchi,
kinachoipa Mamlaka uwezo wa kutoa adhabu kwa Wenye Leseni dhidi ya
uvunjifu wa Sheria, Kanuni na Masharti ya Leseni, Mamlaka ya Mawasiliano
imetoa:
A. Onyo kali kwa Kampuni za:
(i) Benson Informatics Limited (inayojulikana kama Smart),
(ii) MIC Tanzania Limited (inayojulikana kama Tigo),
(iii) Airtel Tanzania Limited,
(iv) Viettel Tanzania Limited (inayojulikana kama Halotel), na
(v) Zanzibar Telecom Limited (inayojulikana kama Zantel).
kwa
kushindwa kutimiza matakwa ya Kanuni ya 8(a) ya Kanuni za Mawasiliano
ya Kielektroniki na Postal ya mwaka 2011 [the Electronic and Postal
Communications (Computer Emergency Response Team) Regulations, 2011] kwa
kushindwa kuweza mazingira salama kwa watumiaji wa huduma za
mawasiliano.
B. Imeamuru Kila Kampuni husika:
(i)
Kuhakikisha kuwa, kuanzia siku ya kutolewa kwa amri hii, inaweka
mazingira salama katika mtandao wake yatakayozuia utumaji wa jumbe za
kilaghai (yaani ‘spoofed messages’) na matishio mengine ya kiusalama;
(ii)
Kulipa faini ya Shilingi za Kitanzania Milioni Ishirini na Tano (Shs
25,000,000.00) kwa Mamlaka ya Mawasiliano kabla ya tarehe 29 Januari,
2016; na
(iii)
Endapo Makamuni haya yatashindwa kutimiza amri Na.2 hapo juu, Mamlaka
itachukua hatua zaidi za kisheria na kiudhibiti dhidi ya Kampuni ya Simu
husika.
7.
Aidha, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapeda kuchukua fursa hii
kuwatahadharisha wananchi kuwa makini na jumbe za kuwataka kutuma fedha
bila ya kuwa na uhakika. Inashauriwa kuhakiki ujumbe husika kwa kupiga
simu na kuongea na mhusika kabla ya kufanya maamuzi ya kutuma fedha hata
kama namba inayotumika unaijua. Vilevile wawe makini wanapopokea jumbe
zinazoonesha zinatoka kwa mtu fulani wanayemjua kumbe ni matapeli
wanaotumia ulaghai kwa njia hii ya “spoofing”.
IMETOLEWA NA
Dkt. Ally Y. Simba
MKURUGENZI MKUU
30 Disemba, 2015




Post a Comment