Siku moja baada ya
kuambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya Leicester City , mkufunzi wa Chelsea
Jose Mourinho sasa anadai wachezaji wanamsaliti
Mourinho anasema wamefanya kila jitihada katika mazoezi kuhakikisha kuwa the blues wanaibuka videdea lakini wapi !''Inachosha sana kutizama kazi ambayo tumefanya ikisalitiwa'' alisema Mourinho.
''Wakati mwengine nahisi kama vile nilijitahidi kuimarisha uwezo wa wachezaji wetu msimu uliopita na sasa inaonekana wameshindwa kustahimili ushindani katika kiwango hicho''alifoka Mourinho.
Msimu uliopita Chelsea walipoteza katika mechi tatu tu walizoshiriki lakini msimu huu, mambo yamewageuka na maji yamezidi unga.
Chelsea walipoteza mechi yao ya 9 msimu huu kati ya 16 walizocheza.
The Blues sasa wamejipata katika nafasi ya 16 wakiwa na alama moja tu zaidi ya timu zinazotishiwa kushushwa daraja msimu ujao.
Mabao ya Jamie Vardy na Riyad Mahrez yaliisaidia 'The Foxes' katika uwanja wao wa nyumbani wa King Power Stadium.
Kinachowashangaza wapenzi wa timu hiyo ni kwanini wachezaji walioishinda ligi msimu uliopita sasa wanashindwa hata kustahimili ushindani kutoka kwa timu ndogo.
Iwapo motisha katika timu ya Chelsea haitaimarika kwa haraka kuna hofu kibarua cha mreno huyo kitaingia mchanga.
Kocha huyo wa Chelsea anakila sababu ya kuwa na hofu haswa wakijiandaa kukabiliana na Sunderland siku ya jumamosi.
''Hatuwezi maliza katika nafasi 4 za kwanza ila tukijitahidi huenda tukacheza katika ligi ya Europa'' alisema Mourinho.
'Naona haya bila shaka'
Post a Comment