0
November 2 shirikisho la soka barani Afrika CAF limetangaza majina 1o ya wachezaji soka wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika sambamba na majina ya wachezaji 10 wengine wanaowania tuzo hiyo kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ya Afrika.
December 14 shirikisho hilo limechuja majina hayo 20 ya wachezaji waliokuwa wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ya Afrika na wachezaji wanaowania tuzo hiyo ya Afrika kwa ujumla, mchujo uliyofanywa na CAF umepelekea kupatikana kwa majina matatu kwa kila upande.
IMG_20151214_212925
Wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika
Majina yaliyotajwa kwa wachezaji wa ndani ya Afrika ni Mbwana Samatta mtanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Robert Kidiaba golikipa wa TP Mazembe na timu ya taifa ya Kongo na  Baghdad Bounedjah wa Algeria anayekipiga katika klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.

Wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa Ligi za ndani.
Lakini kwa upande wa wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ujumla ni kiungo wa mitaifa wa Ivory Coast na klabu ya Man City ya Uingereza Yaya TourePierre – Emerick Aubameyang kutoka Gabon na klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani na Andre Ayew wa Ghana lakini anakipiga katika klabu ya Swansea City ya Uingereza. Tuzo hizo zitatolewa January 7 2016 Abuja Nigeria.


Post a Comment

 
Top