Baada ya dirisha la usajili la Ligi Kuu Uingereza
kufungwa mara nyingi wachezaji wanaosajiliwa kwa dau kubwa huwa
wanaingia katika headlines za kupanda kwa mishahara yao. Miongoni mwa
wachezaji wapya walioingia katika list ya TOP 10 ya mastaa wanaolipwa
mishahara mkubwa ni Raheem Sterling. Stori kutoka sokka.com hii ndio list ya mastaa wa soka wa Uingereza wanaolipwa mishahara mikubwa.
10- Nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry yupo katika list analipwa pound 160000 kwa wiki.
=8- Kevin De Bruyne huyu ni moja kati ya sura mpya zilizojiunga na Man City msimu huu akitokea klabu ya VLF Wolfsburg ya Ujerumani. De Bruyne analipwa pound 170000.
Kevin De Bruyne
8- Nyota wa zamani wa klabu ya Arsenal ya Uingereza ambaye anakipiga katika klabu ya Chelsea ya Uingereza Cesc Fabregas anavuta mshahara wa pound 170000 sawa na Kevin De Bruyne wa Man City.
Cesc Fabregas
7- Raheem Sterling kabla ya uhamisho wake wa pound milioni 49 kutoka Liverpool kujiunga na Man City hakuwa hata katika TOP 20 ya wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa, ila kwa sasa anavuta mshahara wa pound 180000 kutoka Man City..
Raheem Sterling
6- Mfalme wa assist anayekipiga katika klabu ya Arsenal Mesut Ozil anatajwa na mtandao wa sokka.com kuwa analipwa na Arsenal mshahara wa pound 190000 kwa wiki mkwanja.
Mesut Ozil
5- David Silva ambaye anatajwa kuwa ndio kiungo mbunifu katika Ligi Kuu Uingereza, anavuta mshahara wa pound 200000 kwa wiki ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 500 za kitanzania.
David Silva
4- Eden Hazard alikuwa anawaniwa na klabu ya Man United kabla ya mwaka 2012 kuamua kujiunga na Chelsea. Hazard anavuta mkwanja wa pound 220000 kwa wiki.
Eden Hazard
=2- Yaya Toure huyu ndio staa pekee kutoka bara la Afrika anaolipwa mshahara mkubwa katika Ligi Kuu Uingereza analipwa pound 240000 kwa wiki, mshahara ambao ni sawa na mchezaji mwenzake wa Man City Sergio Aguero.
Yaya Toure
2- Sergio Aguero anakamilisha list ya wachezaji watano wa Man City wanaoongoza kwa kulipwa mkwanja mrefu anavuta mshahara wa pound 240000 sawa na Yaya Toure.
Sergio Aguero
1- Wayne Rooney ndio staa wa kwanza anayelipwa mshahara mkubwa Ligi Kuu Uingereza. Rooney anavuta mkwanja wa pound 260000 akiwa na klabu ya Man United. Mshahara wa Rooney
ni zaidi Tsh milioni 600 za kibongo kiwango ambacho ukizidisha mara
wiki nne za mwezi mmoja unapata bilioni 2.4 za kibongo, huo ni mshahara
wa Rooney wa mwezi ambao kwa makadirio ya kawaida bajeti ya vilabu vyote vya Ligi Kuu kiundeshaji wake kwa mwezi mmoja.
Wayne Rooney
Post a Comment