
Tamko
kutoka kwa Balozi Mark B. Childress kuhusu uamuzi wa Bodi ya Shirika la
Changamoto za Milenia kuahirisha kupigia kura mkataba wake na Tanzania
*********
Tarehe
16 Disemba, Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) haikuichagua
Tanzania kwa mkataba wa pili. Bodi iliahirisha kupigia kura mkataba wa
pili, ikisubiri kutatuliwa kwa masuala ya kiutawala.
Bodi
inaweza kuangalia upya ustahilifu wa Tanzania mwaka 2016. Ninatumaini
kwamba Serikali ya Tanzania itachukua hatua hivi karibuni zitakazotatua
masuala hayo ya kiutawala. Halafu, Bodi itaweza kupiga kura kuichagua
tena Tanzania na kuidhinisha maendeleo ya mkataba.
Masuala
ya kiutawala ya Bodi yanaakisi maadili ya muda mrefu ya MCC. Kufutwa
kwa matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar kulisitisha mchakato wa
uchaguzi uliokuwa unaenda vizuri na kwa amani.
Matumizi
ya Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 kuwakamata watu waliokuwa
na kibali halali kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi yalikwaza uhuru wa
msingi wa kujieleza na kukutana.
MCC
imetiwa moyo na hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na Rais Magufuli za
kuimarisha vita dhidi ya ubadhilifu na rushwa. MCC inatumaini kuwa
jitihada hizo zitaendelea na kuleta mabadiliko ya kimfumo.
Mpekuzi blog
Post a Comment