Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akiwasili katika kituo cha Foreplan Clinic kinachotoa
tiba mbadala kilichopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam alipofanya
ziara ya kushtukiza katika kituo hicho jana jioni. Kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi Tiba Asilia na Tiba Mbadala Dk.Paul Mhame kutoka wa Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.(Picha na Geofrey
Adroph wa Pamoja Blog)
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akipokelewa na mmoja wa wauguzi wa kituo hicho ambapo
jina lake halikupatikana kwa haraka baada ya Mkurugenzi wa kituo hicho
Dk. Mwaka Juma Mwaka kutokuwepo kwenye kituo chake cha Foreplan Clinic
kilichopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa baadhi ya wananchi
waliofika kupata matibabu katika kituo cha Foreplan Clinic kuhusu huduma
zitolewazo katika kituo hicho kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka.
Msaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy
L. Mbuya akimtolea ufafanuzi Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuhusu huduma
zitolewazo katika kituo cha Foreplan Clinic mara baada ya kuanza kukagua
kituo hicho kinachotoa tiba mbadala.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikikagua
kifaa kinachotumika kufanyia vipimo kwenye kituo cha Foreplan Clinic
wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho jana jioni
Desemba 14, 2015
Hiki ndicho kifaa kinachotumika kupimia wagonjwa kwenye maabara ya kituo hicho cha tiba mbadala.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwauliza
maswali wasaizizi wa kituo hicho wakiongozwa na Bi Teddy L. Mbuya mara
baada ya kukuta hali ya sintofahamu katika kituo hicho.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akikagua moja
ya dawa zinazotolewa kwa wangonjwa wanaokuja kutibiwa kwatika
kituohicho cha tiba mbadala
Bi. Rozaria Anthony ambaye ni
muhudumu wa dawa akikaa kimya baada ya kuulizwa maswali na Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi
Kigwangalla na kukosa la kujibu.
Hizi ni dawa za asili zinazouzwa katika kituo hicho cha tiba mbadala.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akimpa maelekezo Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na
mbadala Dk.Paul Mhame kutoka Wizara yawa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Na Mwandishi wetu
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis
Kigwangala jana majira ya jioni amefanyaziara ya kushtukiza katika
kituo kinachotoa tiba mbadala cha Foreplan Clinic kinachomilikiwa na Dk.
Mwaka Juma Mwaka kilichopo Ilala Bungoni na kujionea hali halisi ya
kituo hicho.
Mara
baada ya kufika alianza kufanya ukaguzi kuanzia sehemu ya Mapokezi mpaka
kwenye vyumba vya matabibu lakini katika vyumba vyote hakuna daktari
aliyekuwa anatoa huduma.
Akizungumza
na wagonjwa waliokuwa wakisubiria tiba alisema kuna waliofika katika
kituo hicho ili kutibiwa lakini kituo hicho hakina uwezo wa kuwahudumia
wagonjwa hao.
Na kuwataka wagonjwa hao waende kwenye hospitali ili wapate matibabu yanayoendana na magonjwa wanayoumwa.
Akizungumza
msaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya alisema yeye hawezi kusema
kuhusu kituo hicho maana yeye sio msemaji mkuu bali alimwomba Naibu
Waziri kufanya ukaguzi katika kituo hicho pamoja na kuwauliza maswali
wahusika mbalimbali wa vitengo vya kituo hicho.
Baada ya
ukaguzi wa kituo hicho Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amemwagiza Mkurugenzi Msaidizi
Tiba Asilia na Mbadala Dk.Paul Mhame ndani ya wiki moja kufanya ukaguzi
kwa kituo cha Dk. Mwaka na aletewe taarifa iliyokamilika kuhusu taaluma
yeke pamoja na washirika wake na pia dawa anazozitumia kama ni rafiki
kwa wananchi wanaotumia dawa hizo pamoja na kufanya ukaguzi wa vituo
vyote vinavyotoa tiba mbadala na tiba asilia kama Dk. Ndodi, Dk. Rahabu
nk. ili kuwabaini wanaowalaghai wananchi.
Pia
amesema Dk. Mwaka Juma Mwaka amekuwa akijitangaza kupitia vyombo
mbalimbali hapa nchini ambavyo ni kosa la kutangaza kama unafanya kazi
za tiba tabibu.
Alisema madaktari wana miiko na katika miiko hiyo ambayo inatumika na mojawapo ikiwa ni kutojitangaza.
Naibu
waziri aliendelea kusema kuwa Dk. Mwaka amekuwa akijiita Dokta na
amekuwa akichambua mwili wa binadamu kama vile ameusomea udaktari wakati
sheria ya tiba asilia na tiba mbadala hairuhusu watu wa tiba asilia na
Tiba mbadala kutumia maneno ya tiba ya kisasa.
Pia Naibu
Waziri amamtaka Dk. Mwaka Juma Mwaka kufika wizarani leo saa mbili
asubuhi akiwa na nyaraka zake zote zinazohusu utoaji wa huduma ya Tiba
Mbadala kwani amekuwa akijiita majina ya tiba za kisasa na pia kutibu
kwa njia ya kisasa badala ya kutibu kwa njia ya Asilia au Tabibu.
Post a Comment