Wakizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam kwa niaba ya
mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Bi.Victoria Bura amesema ugonjwa
wa kipindupindu imeathiri mikoa mbalimbali ikiwemo mkoa wa Dar es Salaam
ambapo watu 53 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo huku watu 4076
wakidaiwa kuugua ugonjwa huo laktika wilaya tatu za jiji la Dar es
Salaam lakini kwa sasa hali imekuwa nzuri huku mkuu wa kitengo cha elimu
ya afya kwa umma kutoka wizara ya afya na usyawi wa jamii akieleza
juhudi walizofanya katika kuelimisha jamii na kupata matokeo mazuri hadi
sasa kwa nchi nzima.
Dakta Mery Kitambi kutoka kitengo cha dharura na maafa kutoka
wizara ya afya na ustawi wa jamii,amsema watu 106 wamepoteza maisha
kutokana na ugonjwa huo huku watu 7598 wakidaiwa kuugua ugonjwa huo
katika mikoa 17 na wilaya 39 ambazo ugonjwa huo ulifika jitihada nyingi
zimefanyika kupambana na ugonjwa huo hivyo wadau wotee wametakiwa
kushirikina na wizara ya afya katika kupambana na ugonjwa huo kwa
maslahi ya taifa huku halmshauri ya kinondoni nayo ikionekana kuathirika
na ugonjwa huo.ITV
Post a Comment