Mazembe ilipata ushindi wa 2-1 ugenini wiki iliyopita bao moja likifungwa na Samatta ambaye anacheza pamoja na Thomas Ulimwengu, mkali mwingine kutoka Tanzania na sare yeyote itawafanya waweke rekodi ya kutwaa ubingwa wa afrika mara ya kwanza. Kando na kuwania rekodi ya kuwa watanzania wa kwanza kubeba ubingwa huo, Samatta pia ana nafasi kubwa ya kutwaa kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora. Amelingana mabao na Bakri Al-Madina wa El Merreikh ya sudan ambaye timu yake ilishatolewa nusu fainali.
Hii ndio sababu kuna uhakika Samatta atatwaa tuzo hilo kwa vyovyote, mbali na hilo la kunyakua ubingwa, Samatta pia tayari amepata kuorodheshwa kwenye wachezaji kumi bora wanaowania tuzo ya mwanasoka bora afrika zitakapotolewa Nigeria hapo Januari.
Post a Comment