Mamilioni ya watu watabakia katika umasikini ifikapo mwaka 2030, mpaka hatua zitakapochukuliwa, kuzuia hali ya ujoto duniani.
Utabiri uliotolewa na Benki ya Dunia umeonesha uwezekano wa kupanda kwa bei za vyakula barani Afrika kwa asilimia 12.
Zaidi ya mamilioni ya watu watakuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa malaria, na pia tatizo la wahamiaji haramu litaongezeka.
Onyo hili
limekuja wakati, Mawaziri kutoka nchi sabini wakianza mkutano wao
kujaribu kukamilisha mpango wa kuweza kudhibiti gesi chafu viwandani.
Makubaliano
yoyote yatakayofikiwa yatawasilishwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa
wa Hali ya Hewa utakaofanyika mwezi ujao mjini Paris Ufaransa.
Post a Comment