Maafisa walizingira sehemu ya mtaa wa Saint Denis wakisaka washukiwa wa mashambulio ya Ijumaa
Washukiwa wawili
wamefariki baada ya maafisa wa usalama kushambulia Saint Denis kaskazini
mwa Paris, wakisaka waliohusika mashambulio ya Ijumaa.
Maafisa kadha wa polisi wamejeruhiwa kwenye operesheni hiyo, kituo cha runinga cha BFMTV cha Ufaransa kimeripoti.
Video iliyoonyeshwa na vituo vya televisheni vya BFMTV na iTele zimeonyesha watu walioshuhudia wakisema milio ya risasi ilianza kusikika saa kumi unusu alfajiri saa za Ufaransa.
Naibu meya Stephane Peu amewahimiza raia wasalie manyumbani, akisema "hili si shambulio jipya bali ni operesheni ya polisi".
Watu 129 walifariki kwenye mashambulio yaliyotokea maeneo sita mjini Paris.
Kundi la Islamic State (IS) limesema ndilo lililotekeleza mashambulio hayo.
Ripoti moja inasema barabara zimefungwa eneo la Place Jean Jaures mtaa wa Saint Denis.
Post a Comment