Figo ni miongoni mwa viungo muhimu katika mfumo wa utendaji
kazi wa mwili wa binadamu. Mwili wa binadamu una figo mbili zenye maumbo
yanayofanana, yakiwa yamejificha nje ya utando unaozunguka tumbo, chini kidogo
ya mbavu. Ugonjwa wa figo ni tatizo kubwa kwa watu wengi,ugonjwa huu si tu
unaleta maumivu kwa mgonjwa,bali pia hautibiki kirahisi pamoja na gharama za
matibabu husika kuwa kubwa na wengi kushindwa kuzimudu.
VISABABISHI VYA
UGONJWA WA FIGO
1.Matumizi mabaya ya dawa hasa za maumivu kama
diclofenac na madawa mengine ya maumivu.
2.Uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe kupita kiasi
KAZI ZA FIGO
1. Kuchuja vitu mbalimbali pamoja na sumu katika damu,
kusaidia kuhifadhi,kudhibiti kiwango cha maji na madini (electrolytes) mwilini.
Figo huchuja vitu hivyo pamoja na maji yaliyo mwilini na
kutengeneza mkojo, huchuja pia maji yasiyohitajika mwilini huku yakinyonya
madini na kemikali muhimu kuzirudisha katika mzunguko wa damu na kutoa nje
uchafu usiohitajika.
2. Kusaidia kutengeneza kiasili cha erythropoletin ambacho
ni muhimu katika utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu, hupokea
asilimia 25 ya damu na kila figo ina chembechembe hai ndogo milioni moja, pia
kusaidia kudhibiti na kurekebisha shinikizo la damu mwilini (blood pressure).
AINA ZA UGONJWA WA
FIGO.
ZIPO AINA MBILI ZA
UGONJWA WA FIGO
1.Aina ya `kwanza figo kushindwa kufanya kazi kwa ghafla na
muda mfupi.
2. Aina ya pili ni ile ya figo kushindwa kufanya kazi
polepole na kwa muda mrefu.Figo huharibiwa taratibu na kuendelea kupunguza
uwezo wake wa kufanya kazi kadiri siku zinavyokwenda.Figo kushindwa kufanya
kazi polepole na kwa muda mrefu.
SABABU ZA FIGO
KUSHINDWA KUFANYA KAZI KWA GAFLA
1. Kupungua kwa mzunguko wa damu kwenye figo, kemikali za
mwilini au kushambuliwa na sumu. Sababu za figo kushindwa kufanya kazi ghafla
2.Ugonjwa wa moyo, moyo kushindwa kusukuma damu kwa ghafla,
au waliougua maradhi ya moyo kwa muda mrefu.
3.Sababu zinazofanya figo ishindwe kufanya kazi taratibu na
kwa muda mrefu na hatimaye kushindwa kabisa kuwa ni presha kuwa juu, kisukari,
magonjwa yanayosababishwa na bakteria, HIV, saratani na sumu mbalimbali
zinazoingia mwilini.
DALILI ZA FIGO
KUSHINDWA KUFANYA KAZI.
1.Dalili ya kwanza ni kupungua kwa kiasi cha mkojo,
kushindwa kupumua, kusikia kichefuchefu, kutapika na kuvimba miguu.
2.Dalili nyingine ni maji kujaa mwilini, madini ya mwili
kuwa juu hasa ya ‘potashiamu’, asidi nyingi, matatizo katika moyo, ubongo,
kukosa hamu ya kula na kudhoofika mwili.
3. Dalili nyingine kwa wagonjwa ambao hawagunduliki mapema
ni kuvimba macho wakati wa asubuhi na uvimbe kupungua baadaye.
4. Dalili nyingine ni kuvimba miguu asubuhi, kupungukiwa
damu mwilini kama dalili za kwanza (kwani figo
ikishindwa kufanya kazi ya kusaidia kutengeneza damu).
Post a Comment