|
Bei ya korosho kwa msimu wa 2015/2016 imeongezeka nakufikia shilingi 2,620 kwa kila kilo moja,ikilinganishwa na bei ya shilingi 1,460.00 kwa msimu wa 2014/2015.
Hayo yameelezwa na meneja mkuu wa chama kikuu cha ushirika cha RUNALI,Christopher Mwaya alipozungumza na timu
ya waandishi wa habari ofisini kwake mjini Nachingwea mwanzoni mwa wiki hii.
Mwaya,alizitaja sababu za ongezeko hilo la bei kuwa ni uzalishaji mdogo wa zao hilo uliosababishwa na hali ya hewa.Ikiwamo mvua kuwa kidogo ukilingamisha msimu uliopitana,
Aliitaja sababu nyingine kuwa ni ongezeko la wanunuzi."Mwaka jana kulikuwa na kampuni 28 lakini mwaka huu zipo 76,
na kipindi cha harakati za uchaguzi serikali ilijikita zaidi kwenye uchaguzi ndipo walanguzi walipata mwanya wakununua korosho nakwenda kuuzia nje ya wilaya na mkoa .
Alibainisha kuwa kiwango cha uzalishaji katika msimu huu kitapungua kwatani 11,500,ikilinganishwa na tani 23000 zilizozalishwa na kuuzwa msimu uliopita.
Aidha Mwaya pamoja na changamoto za uzalishaji lakini chama pia kinakabiliwa
changamoto Ikiwamo baadhi ya vyama vya msingi vya ushirika kushindwa kulipa ushuru
|
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment