JESHI la
Polisi mkoani Tanga limemfukuza kazi kwa kosa la fedheha aliyekuwa
askari wake katika Kikosi cha Usalama Barabarani, Koplo Anthony Temu
(46) wa Kituo cha Polisi Kabuku wilayani Handeni.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Zuberi Mwombeji, kufukuzwa
kwa askari huyo kumetokana na taarifa ya kuomba na kupokea rushwa
iliyopatikana kupitia mitandao ya kijamii.
Alisema
Novemba 9, mwaka huu saa 7.30 mchana kupitia mitandao ya kijamii,
alionekana askari mmoja wa kikosi cha usalama barabarani akipokea rushwa
kutoka kwa dereva wa gari alilokuwa amelisimamisha kutokana na makosa
ya usalama barabarani.
Alisema;
“Katika ufuatiliaji ilibainika kwamba eneo la tukio ni katika kijiji na
kata ya Kitumbi iliyopo wilayani Handeni Mkoa wa Tanga katika Barabara
Kuu ya Segera- Chalinze … askari aliyebainika kutenda kosa hilo ni F.
785 Anthony Temu na kutokana na uzito wa kosa lenyewe alichukuliwa hatua
za haraka za kinidhamu.
“Amekamatwa
na tayari mashitaka ya kijeshi yameendeshwa dhidi yake na kutiwa
hatiani ambapo amepewa adhabu ya kufukuzwa kazi kwa fedheha … hivi
ninavyoongea nanyi hapa ameshafukuzwa kazi si askari tena tangu jana
(juzi) jioni.”
Alisisitiza
mtuhumiwa huyo ameshakabidhiwa kwa maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na kielelezo ambacho ni video
iliyokuwa ikirushwa kwenye mitandao ya kijamii ili waendelee
kumshughulikia kwa upande wa jinai katika makosa ya kuomba na kupokea
rushwa.
Hata
hivyo, alisema Polisi mkoani Tanga inawashukuru wananchi hao walioibua
taarifa hizo na kuwataka kuliarifu kuhusu matukio yoyote yanayohusisha
ukiukwaji wa maadili katika jeshi hilo.
Tumechunguza taarifa zile na tumemtafuta tumemshughulikia na kumkabidhi kwa maafisa wa TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi sababu wao ndio wanashughulika na maswala haya ya rushwa‘ – Kamanda Mwombeji.
Tumechunguza taarifa zile na tumemtafuta tumemshughulikia na kumkabidhi kwa maafisa wa TAKUKURU wanaendelea na uchunguzi sababu wao ndio wanashughulika na maswala haya ya rushwa‘ – Kamanda Mwombeji.
Post a Comment