Idadi kubwa ya wahamiaji haramu wanaosafiri katika mazingira magumu katika bahari ya mediterenia kunatia wasiwasi nchi za Ulaya.
Zaidi
ya wahamiaji laki saba wameingia katika bara la Ulaya kupitia njia ya
bahari katika kipindi cha mwaka 2015, hayo ni kwa mujibu wa shirika la
kimataifa la uhamiaji.Huku maelfu wengine wakiripotiwa kupoteza maisha wakati wakiwa katika safari hizo mwaka huu.
Kutokana na maafa hayo, mkutano unaofanyika nchini Malta unalenga zaidi kutatua changamoto lakini pia kuangalia fursa zitokanazo na uhamiaji.
Majadiliano miongoni mwa wajumbe yatalenga katika nyanja mbalimbali ikiwemo kujenga mwelekeo wa pamoja wa kukabiliana na matatizo kama vile uhamiaji haramu na biashara haramu ya watu.
Inaaminika kwamba, umaskini uliokithiri, ukosefu wa haki na migogoro ya kisiasa kwa muda mrefu imekuwa ndio chanzo cha uhamiaji kutoka barani Afrika kuelea Ulaya.
Wataalamu wanasema kwamba, iwapo migogoro ya kisiasa itaendelea kuwepo katika nchi kama vile Libya, Somalia na Eritrea, hivyo jitihada za kukabiliana na wimbi la uhamiaji hazitakuwa rahisi.
Umoja wa Afrika, na Jumuia ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS zitahudhuria ili kutoa misaada zaidi kwa nchi ambazo ndio chanzo kikubwa cha uhamiaji.
Wakati huo huo, tume ya umoja wa ulaya inataka kutoa mamilioni ya Euro kwa nchi za kiafrika ambazo zitakubali kuwapokea wahamiaji ambao hawana sababu za msingi za kuomba hifadhi barani Ulaya.
Post a Comment