Stars imeondoshwa kwa jumla ya mabao 9-2 baada ya kucheza michezo miwili, mchezo wa kwanza Stars ililazimishwa sare ya kufungana kwa goli 2-2 na Algeria jijini Dar es Salaam huku mchezo wa pili uliopigwa Blida, Algeria ukimalizika kwa Stars kulala kwa goli 7-0.
Algeria walianza kupata bao la kwanza sekunde ya 40 kupitia kwa Yacine Brahimi huku Ghoulam Faouzi akipachika goli la pili dakika ya 23 kabla ya Ryad Mahrez kutupia la tatu dakika ya 43 na kuufanya mchezo kwenda mapumziko Algeria wakiwa mbele kwa magoli 3-0 dhidi ya Stars.
Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mabadiliko kwa kuwatoa Farid Musa na nafasi yake kuchukuliwa na Salum Telela wakati Aishi Manula aliingia kuchukua nafasi ya Ali Mustafa.
Dakika ya 49 Algeria waliendeleza mvua ya magoli kwa Stars baada ya Slimani Islam kuipatia Algeria bao la nne kwa mkwaju wa penati wakati Ghoulam Faouzi akiifungia Algeria tano pia kwa mkwaju wa penati ikiwa ni dakika ya 59.
Carl Medjani akafunga goli la sita dakika ya 72 huku Slimani Islam akipachika bao la saba dakika ya 75.
Farid Musa, Himid Mao Mkami, Kelvin Yondani, Haji Mwinyi Nadir Haroub na Aishi Manula walioneshwa kadi ya njano huku Mudathir Yahya akioneshwa kadi mbili za njano zilizopelekea kupata kadi nyekundu dakika ya 41 kipindi cha kwanza na kuiacha Stars ikicheza pungufu kwa muda wote uliosalia.
GOOOOOOOOO Dk 72, Carl anaifungia Algeria bao la sita tena kwa ulahisi kabisa kwa kuwa alibaki peke yake
Dk 65, Samatta anasogezewa na Mwinyi lakini anapiga shuti mlenda kabisa
KADI Dk 62, Medjan Carl analambwa kadi ya njano kwa kumpiga pepsi Himid Mao. Hata hivyo awali alimpa kadi Sliman na akagundua amekosea baada ya kuelekezwa na Cannavaro
Dk 61, Kapombe anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa Mahrez na kuwa kona lakini haina madhara
GOOOOOOOO Dk 58 Ghoulan Fouz anafunga mkwaju wa penalti
PENAAAAT Dk 57, Aishi anamgonga mchezaji wa Algeria, mwamuzi anasema penat
Dk 54, Aishi anafanya kazi ya ziada kudaka shuti la Mahrez
Dk 53, Mwinyi anaupata mpira, anapiga chenga na kupiga shuti lakini dhifu kabisa
Dk 52, Samatta anawatoka mabeki wa Algeria, anapiga shuti lakini linawababatisha mabeki
GOOOOOOOO Dk 48 Slimani anapiga penalti, anafunga bao kwa mkwaju wa penalti
PENAAAAAT Dk 47, Yondani anasakiziwa mzigo wa penalti lakini aliangushwa yeye lakini mwamuzi akajikausha, alipomgusa yeye na kuanguka, mwamuzi kafunika
Dk 46, Stars wanamtoa Barthez nafasi yake inachukuliwa na Aishi Manula, pia anaingia Salum Telela kuchukua nafasi ya .....
MAPUMZIKO.
GOOOOOO Dk 42 Marhez Ryad anaifungia Algeria bao la tatu kwa ulaini kabisa
KADI NYEKUNDU Dk 41, Mudathiri anapata kadi ya pili ya njano, tena ya kijinga kabisa. Analambwa kadi nyekundu
KADI Dk 38, Mwinyi analambwa kadi ya njano ya kipuuzi kabisa
SUB Dk 36 Algeria wanamtoa Bentaleb anaingia Adiane Guedioura
Dk 33, Algeria wanapata kona, inachongwa na Brahimi anauwahi mpira na kutoa krosi safi, lakini Bentaleb anapiga shuti kuuuuubwaa
Dk 29, Riad anaingia katika eneo la hatari la Stars anapiga shuti huku mabeki wa Stars wakiwa wamezubaa lakini mpira unatoka nje
Dk 27, Maguri anafunga kwa shuti kali kabisa lakini mwamuzi msaidizi anasema ni off side
Dk 26, Bentaleb analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Mudathiri
Dk 26, Kipa Rais anafanya kosa kwa kupiga mpura anaouwahi Samatta, lakini anapiga shuti mtoto kabisa
DK 23 Fauz anayekipiga Napoli ya Italia anafunga bao la pili kwa Algeria baada ya kupiga mpira adhabu unaomshinda Barthez
KADI Dk 22, Mudathir analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ibrahimi
Dk 19, Cannavaro anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa kichwa uliokuwa umemlenga Ali
KADI Dk 17, Himid analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Bentaleb
Dk 11, Algeria wanapata kona, inachongwa na Brahimi lakini Cannavaro anaokoa
KADI Dk 5 Kapombe anapewa kadi ya njano kwa kumuangusha Brahimi
GOOOOO Dk 1, Sliman anatoa krosi nzuri kwa Brahimi ambaye anafunga kwa ulaini kabisa.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.